Mkuu mpya wa baraza la kijeshi mpito nchini Sudan amesema leo kuwa serikali ya kiraia itaundwa baada ya mashauriano na makundi ya upinzani na kuahidi kuwa kipindi cha mpito kitadumu kwa muda usiozidi miaka miwili.

Wakati wa hotuba yake ya kwanza kwa njia ya televisheni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza pia kuondoa marufuku ya kutembea usiku na kuamuru kuachiwa huru kwa watu wote waliofungwa chini ya sheria ya hali ya hatari iliyowekwa na utawala ulioangushwa. Wakati huo huo mkuu wa idara ya ulinzi na ujasusi nchini Sudan amejiuzulu leo siku moja baada ya Jenerali Awad Ibn Auf kutangaza kuwachia wadhifa wa kiongozi wa mpito kutokana na shinikizo la waandamanaji. Salah Abdallah Mohamed Saleh ambaye alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa wakati wa utawala wa rais Bashir amekuwa akituhumiwa kufanya mauaji ya waandamanaji wanaotaka kukomesha utawala wa jeshi kwenye kipindi cha mpito. Shirika la habari la taifa SUNA limeripoti kuwa kiongozi mpya wa mpito Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ameridhia kujiuzulu kwa bwana Salah.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili ya DW

Latest News

Idadi ya waliokufa ajali ya boti DRC yafikia 40
21 Apr 2019 10:10 - Kisali Shombe

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong [ ... ]

Kenya wang'ara Ngorongoro Marathoni.
20 Apr 2019 14:52 - Kisali Shombe

Mwamko mdogo miongoni mwa wanariadha wa Tanzania umewafanya wanariadha wa kenya kutamba katika mashindano ya Ngorongoro  [ ... ]

Wamisri wapiga kura kumuongezea muda Rais Abdel Fattah al-Sisi
20 Apr 2019 14:43 - Kisali Shombe

Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.