Maalfu ya watu wameshiriki katika maandamano makubwa kabisa, kuwahi kufanyika hadi sasa nchini Sudan ya kumtaka Rais wa nchi hiyo Omar al-Bashir ang’atuke baada ya kutawala kwa muda wa takriban miaka 30.

Waandamanaji walikwenda hadi kwenye makao makuu ya jeshi mjini Khartoum, huku wakipaza sauti zao wakisema, amani, haki na uhuru. Makaazi ya rais al-Bashir pia yamo kwenye makao makuu hayo. Waandaaji wamesema kabla ya maandamano hayo kuanza idadi kubwa ya polisi waliwekwa katika sehemu mbalimbali za mji mkuu, Khartoum ambapo waliwazuia wapita njia kuzifikia sehemu kadhaa za mji huo. Kwa mujibu wa taarifa maandamano hayo yalifanyika kwa usalama. Tangu kuanza harakati za wananchi, mnamo mwezi Desemba za kumtaka rais al-Bashir aachie ngazi, watu 31 wameshauawa. Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watche limesema linaamini kwamba watu 51 waliuawa wakiwemo watoto na wahudumu wa afya.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Idadi ya waliokufa ajali ya boti DRC yafikia 40
21 Apr 2019 10:10 - Kisali Shombe

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong [ ... ]

Kenya wang'ara Ngorongoro Marathoni.
20 Apr 2019 14:52 - Kisali Shombe

Mwamko mdogo miongoni mwa wanariadha wa Tanzania umewafanya wanariadha wa kenya kutamba katika mashindano ya Ngorongoro  [ ... ]

Wamisri wapiga kura kumuongezea muda Rais Abdel Fattah al-Sisi
20 Apr 2019 14:43 - Kisali Shombe

Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.