Msumbiji: Misaada yaanza kuwafikia waliokumbwa na maafa ya kimbunga Idai

Watu walionusurika maafa yaliyosababishwa na kimbunga Idai kilichokumba eneo la Kusini mwa Afrika wameanza kupatiwa misaada ya haraka ya dawa, chakula na mahema.

Kwa mujibu wa taarifa mafuriko yameanza kupungua. Maalfu ya watu waliokuwa wamekwama wiki iliyopita sasa wanapelekwa kwenye sehemu zenye usalama zaidi. Hata hivyo Shirika la Msalaba Mwekundu limetahadharisha juu ya hatari ya kuzuka maradhi ya kuambukiza. Kimbunga Idai kiliukumba mwambao wa Msumbiji na sehemu za Mashariki mwa Zimbabwe na kusabaisha vifo vya watu 700 katika nchi hizo mbili. Na nchini Malawi watu wapatao 56 walikufa kutokana na kimbunga hicho.

Chanzo: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Idadi ya waliokufa ajali ya boti DRC yafikia 40
21 Apr 2019 10:10 - Kisali Shombe

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong [ ... ]

Kenya wang'ara Ngorongoro Marathoni.
20 Apr 2019 14:52 - Kisali Shombe

Mwamko mdogo miongoni mwa wanariadha wa Tanzania umewafanya wanariadha wa kenya kutamba katika mashindano ya Ngorongoro  [ ... ]

Wamisri wapiga kura kumuongezea muda Rais Abdel Fattah al-Sisi
20 Apr 2019 14:43 - Kisali Shombe

Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.