Idadi ya vifo vilivyosababishwa na mafuriko yalioambatana na kimbunga Idai imeongezeka na kufikia watu 217 huku takriban watu 15,000 wakihitaji huduma za uokozi.

 Waziri wa ardhi na mazingira wa Msumbiji Celso Correia amesema hii leo kwamba watu 3,000 tayari wamekwishaokolewa. Wafanyakazi wa kutoa misaada walipambana kuwasaidia manusura lakini pia kuwafikishia misaada ya kiutu nchini Zimbabwe, Malawi na Msumbiji ambazo zimeathiriwa pakubwa na kimbunga hicho. Baadhi ya vyombo vya habari vinaripoti kwamba zaidi ya watu 300 wamefariki kutokana na janga hilo ikiwa ni siku tano baada ya kimbunga hicho Idai kupiga eneo kubwa la Zimbabwe na Malawi. Kimbunga Idai kilianza kwa kuupiga mji wa bandari wa Beira nchini Msumbiji Alhamisi iliyopita na kisha kuelekea nchini Zimbabwe na Malawi na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo na kuyaweka hatarini maisha ya maelfu ya wakazi.

 

Chanzo: kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW

Latest News

Idadi ya waliokufa ajali ya boti DRC yafikia 40
21 Apr 2019 10:10 - Kisali Shombe

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong [ ... ]

Kenya wang'ara Ngorongoro Marathoni.
20 Apr 2019 14:52 - Kisali Shombe

Mwamko mdogo miongoni mwa wanariadha wa Tanzania umewafanya wanariadha wa kenya kutamba katika mashindano ya Ngorongoro  [ ... ]

Wamisri wapiga kura kumuongezea muda Rais Abdel Fattah al-Sisi
20 Apr 2019 14:43 - Kisali Shombe

Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.