Msumbuji imeanza leo siku tatu za maombolezi ya kitaifa baada ya kimbunga kikali kilichoandamana na mafuriko kuwauwa mamia ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa katika maeneo mengi ya kusini mashariki mwa Afrika.

Kimbunga Idai, ambacho kiliupiga mji wa bandari wa Beira mchini Msumbiji Alhamisi iliyopita kabla ya kuingia maeneo ya ndani, kiliandamana na upepo mkali ulovuma kwa kasi na kuvunja majengo na kuyaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu. Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amesema kimbunga hicho kimewauwa zaidi ya watu 200 nchini Msumbuji lakini miili bado inaendelea kupatikana. Katika nchi jirani Zimbabwe, idadi rasmi ya vifo ni watu 98 lakini inatarajiwa kuongezeka kwa sababu mamia ya watu hawajulikani waliko. Wakati huo huo, msaada wa kimataifa umeanza kutolewa katika nchi za Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kufuatia kimbunga hicho.

 

Chanzo; DW Swahili

Latest News

Idadi ya waliokufa ajali ya boti DRC yafikia 40
21 Apr 2019 10:10 - Kisali Shombe

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong [ ... ]

Kenya wang'ara Ngorongoro Marathoni.
20 Apr 2019 14:52 - Kisali Shombe

Mwamko mdogo miongoni mwa wanariadha wa Tanzania umewafanya wanariadha wa kenya kutamba katika mashindano ya Ngorongoro  [ ... ]

Wamisri wapiga kura kumuongezea muda Rais Abdel Fattah al-Sisi
20 Apr 2019 14:43 - Kisali Shombe

Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.