Mkuu mpya wa baraza la kijeshi mpito nchini Sudan amesema leo kuwa serikali ya kiraia itaundwa baada ya mashauriano na makundi ya upinzani na kuahidi kuwa kipindi cha mpito kitadumu kwa muda usiozidi miaka miwili.

Wakati wa hotuba yake ya kwanza kwa njia ya televisheni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza pia kuondoa marufuku ya kutembea usiku na kuamuru kuachiwa huru kwa watu wote waliofungwa chini ya sheria ya hali ya hatari iliyowekwa na utawala ulioangushwa. Wakati huo huo mkuu wa idara ya ulinzi na ujasusi nchini Sudan amejiuzulu leo siku moja baada ya Jenerali Awad Ibn Auf kutangaza kuwachia wadhifa wa kiongozi wa mpito kutokana na shinikizo la waandamanaji. Salah Abdallah Mohamed Saleh ambaye alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa wakati wa utawala wa rais Bashir amekuwa akituhumiwa kufanya mauaji ya waandamanaji wanaotaka kukomesha utawala wa jeshi kwenye kipindi cha mpito. Shirika la habari la taifa SUNA limeripoti kuwa kiongozi mpya wa mpito Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ameridhia kujiuzulu kwa bwana Salah.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili ya DW

Latest News

Tanzania imetia saini Mkataba wa kupatiwa fedha za Msaada wa Shilingi Bilioni 60...
24 Jun 2019 12:35 - Kisali Shombe

Tanzania imetia saini Mkataba wa kupatiwa fedha za Msaada wa Shilingi Bilioni 60 za kitanzania kutoka Serikali ya Watu w [ ... ]

Utata Bandari ya Bagamoyo
24 Jun 2019 11:32 - Kisali Shombe

Siku chache baada ya Rais, Dk; John Magufuli kutangaza Msimamo wa kusitisha ujenzi wa Mradi mkubwa wa Bandari ya Bagamoy [ ... ]

Kizungumkuti, ununuzi wa Pamba, Bukombe.
21 Jun 2019 13:29 - Kisali Shombe

Wilaya ya Bukombe imetoa maazimio kwa wanunuzi wa pamba kuwa ifikapo juni 24 Kampuni itakayoshindwa  kununua vituo vya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.