Katika  jitihada  za kukabiliana  na  uvamizi  wa  tembo  kwenye  mashamba  ya   wananchi    mkoani  Rukwa, wakala  wa    hidfadhi za mistu  wilayani  kalambo  wameanzisha  mradi  wa  ufugaji  nyuki  ambao  utasaidia   wananchi  kujikwamua  na  hali  ya  kiuchumi  sambamba  na kufukuza  tembo kwenye mashamba   yao.

Kumekwepo  na malalamiko   ya  muda  mrefu  kutoka  kwa   wananchi  wa   kata  za Kisumba  na  Pombwe   wilayani  Kalambo   juu  ya  tembo  kuvamia  mashamba  yao  kisha   kuharibu  mazao na  kupelekea   serikali  wilayani  humo  kupitia  wakala   wa  hifadhi  za misitu  kubuni  njia   mpya   ya  kupambana  na  tembo hao kwa  kuanzisha  mradi  wa  ufugaji  nyuki.

Hayo yameelezwa wakati akisoma  akisoma  risala  fupi  mbele   ya  kiongozi   wa   mbio  za Mwenge Venansi  Sinkala  wakati  wa  uzinduzi  wa  mradi  huyo unayo shirikisha  vikundi vitano , amesema mizinga 100 yenye thamani  ya  shilingi  million  nane  imekwisha  kutundikwa   tayari.

kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, haji abdulla hamad amewashauri wananchi kuendelea kutumia mbinu mbadala za kutumia misitu kwa faida kama kufuga nyuki ili kutunza vyanzo vya maji ili kufikia malengo ya serikali ifikapo mwaka 2025.Awali  akiupokea  mwenge  huo . mkuu  wa  wilaya  ya  Kalamnbo  Julieth  Binyura , amesema   mwenge  wa  uhuru  utazindua   miradi  9 yenye thamani  yua  shilingi  billion  1.2.

Latest News

Idadi ya waliokufa ajali ya boti DRC yafikia 40
21 Apr 2019 10:10 - Kisali Shombe

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong [ ... ]

Kenya wang'ara Ngorongoro Marathoni.
20 Apr 2019 14:52 - Kisali Shombe

Mwamko mdogo miongoni mwa wanariadha wa Tanzania umewafanya wanariadha wa kenya kutamba katika mashindano ya Ngorongoro  [ ... ]

Wamisri wapiga kura kumuongezea muda Rais Abdel Fattah al-Sisi
20 Apr 2019 14:43 - Kisali Shombe

Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.