Kocha mkuu wa timu ya Taifa wa Tunisia Nabail Malou amesema Uzoefu ni muhimu na ndio unawapa faida England wakiwa washindani wao wa kwanza katika kombe la dunia tofauti na Tunisia amabao hadhanai kama kunamchezaji hata mmoja ambae amewahi kucheza kombe la Dunia kabla.

Tunisia amabao walishindwa kufuzu kombe la Dunia kwa Makala mbili mfululizo watakuwa na kazi ya ziada kupambana na jeshi la England katika mchezo wa kundi G Japo kocha wao amesisitiza bado hawatawahofia England licha ya ugumu wa mchezo.

Kwa upande wa meneja wa England Gareth Southgate amesema wamefanyia kazi mabadiliko ya mifumo tofauti ya uchezaji lengo ni kupata matokeo lakini pia kutoa burudani kwa kandanda safi watakalo cheza.

Tunisia tangu mwaka 2006 wamekuwa wakitolewa katika hatua za makundi tu katika ushiriki wa Kombe la Dunia pengine mchezo wa leo dakika chache zijazo zinaweza kutuliza mioyo ya Afrika baada ya vigogo wote waliotangulia kupoteza michezo ya kwanza.

Tunisia na England mara ya mwisho kukutana ilikuwa katika mchezo wa ufunguzi hatua ya makundi mwaka 1998 katika kombe la Dunia marseile Ufaransa na England ikawazaba Tunisia mabao 2-0.

Picha na mtandao.

Latest News

Idadi ya waliokufa ajali ya boti DRC yafikia 40
21 Apr 2019 10:10 - Kisali Shombe

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya boti katika Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong [ ... ]

Kenya wang'ara Ngorongoro Marathoni.
20 Apr 2019 14:52 - Kisali Shombe

Mwamko mdogo miongoni mwa wanariadha wa Tanzania umewafanya wanariadha wa kenya kutamba katika mashindano ya Ngorongoro  [ ... ]

Wamisri wapiga kura kumuongezea muda Rais Abdel Fattah al-Sisi
20 Apr 2019 14:43 - Kisali Shombe

Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.